Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, neema na baraka nyingi atujaliazo kila siku hadi tumehitimisha Kongamano letu. Tunamshukuru pia kwa zawadi ya miaka 2025 ya Kuzaliwa Mwokozi wetu Yesu Kristo ambaye ni zawadi ya Matumain i kwetu sisi wanadamu.
Washiriki
Kongamano letu limefanyika kwa siku Tano na walikusanyika watoto 902 na walezi wao 74 kutoka Parokia zote za Jimbo Katoliki la Mafinga
Mada na Wakufunzi
Mada zilizowasilishwa ni kama ifuatavyo: Wito – Sr. Kil iana Sanga (CST), Mashirika ya Kipapa -Sr. Anagladness Mrumah (C.O.L.U, Fadhila – Pd. Gosbert Mlambia, Ulinzi na Usalama wa Watoto – Pd. Martin Mhavile, Yubilei Kuu 2025 – Pd. Paulo Wissa.
Mafanikio
Watoto walifanikiwa kupata mafundisho juu ya Mashirika ya Kipapa, Wito, Fadhila Ulinzi na Usalama wa Mtoto na Dhamira ya Ybilei Kuu 2025. Pia watoto wamepata Sakramenti ya Kitubio na kuhimizwa juu ya majiundo kiroho na Kimaadili. Vilevile watoto walikula, walicheza, kuimba na kusali pamoja kwa furaha. Tukiongozwa na Baba Askofu wetu, Vincent Cosmas Mwagala, tuliadhimisha 03/01/2025 Sherehe ya Watoto Mashahidi ikiwa ni Kilele cha Kongamano na Adhimisho la Yubilei Kuu 2025 Kijimbo katika kundi la Watoto. Hakika tuliona uwepo wa Utukufu na Upendo wa Mungu kati ya watoto katika furaha yao ya kukusanyika Pamoja ndani ya Uzuri wa Mtoto Yesu. Furaha na Shangwe zilitanda Siku zote tano za Kongamano letu.
Imeandaliwa na: Pd. Gosbert Mlambia, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa- Jimbo