Kuanzia tarehe 26 Desemba 2024, Parokia mbalimbali za jimbo la Njombe; wamefanya makongamano ya Utoto Mtakatifu. Katika Parokia ya Familia Takatifu-Utalingolo watoto walifundishwa mada zifuatazo: Haki na wajibu wa mtoto-iliyotolewa na Arodia Mkinga, Mtoto mmisionari-ilitolewa na Sr. Lucia Mpete OSB, Liturjia – Pd. Lucas Mgaya
Kulikuwa na mada zilizotolewa kwa walezi: Namna ya kuwafundisha watoto– Sr. Lucia Mpete OSB, Ulinzi na usalama wa mtoto-Arodia Mkinga
Dhamira kuu ya kongamano ilikuwa: Sisi Sote ni Wamisionari.
Jumla ya watoto washiriki katika Parokia mbalimbali ni 1,794 kadiri ya ripoti zilizotumwa katika Ofisi yetu ya PMS Jimbo. Katika kongamano hili, watoto walipata fursa ya kutembelea watoto walemavu na maskini na kuwapelekea zawadi ndogondogo.
Imeandaliwa na: Pd. Lukas Mgaya, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa-Jimbo