Mwaka huu kongamano la utoto mtakatifu katika jimbo la Ifakara, limefanyika katika parokia ya mtakatifu Francis Xavery Kisawasawa kuanzia tarehe 26-28 Disemba 2024. Kongamano hili lilikuwa na jumla ya washiriki watoto wapatao 591. Kauli mbiu ya kongamano hili ilikuwa ni Mtoto ni Malezi. Aidha, mada mbalimbali ziliwasilishwa na watu wafuatao: Uelewa juu ya Biblia Takatifu na Maadili Mema na Pd. Boniface Mwanja, Sakramenti za Kanisa na Ekaristi takatifu Pd. Edson Lyabonga.
Kongamano hili pia lilinogeshwa na maandamano ya kimisionari ambayo yalifanyika siku ya tarehe 28 na kupokelewa na baba Askofu Salitarus Libena, na baadaye misa takatifu ya Watoto Mashahidi.
Tunamshukuru sdana Mungu aliyeyawezesha haya yakaweza kufanyika kwa kadiri ya mpango wake.
Imeandaliwa na: Pd. Michael Mhina, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa, Jimbo