Kongamano la utoto Mtakatifu lilifanyika Katika Parokia ya Mt. Francisco wa Assis Mwanjelwa huku tukitumia majengo ya Chuo Kikuu (CUoM) Kwa malazi na vipindi kwa watoto wetu. Kaulimbiu ya Kongamano letu ni “ULINZI WA MTOTO NI JUKUMU LANGU NA LAKO

Idadi ya washiriki ilikuwa kama ifuatavyo; Watoto wa Kipapa 2908, Mapadre 5, Watawa 15, Walezi 241 na Askofu 1

 

Tulianza Kongamano kwa Misa Takatifu iliyoongozwa na Mhasham Askofu Msaidizi Godfrey mwasekaga mnamo tarehe 28.12.2024 asubuhi kisha ikafuata rariba ya vipindi mbalimbali. Mada zilizofundishwa ni pamoja na;

  1. Ulinzi wa Mtoto (Mapadre, Watawa, RPC na wadau waalikwa)
  2. Mtoto na sala (Mapadre na Watawa walioandaliwa)
  3. Ekaristi Takatifu chemichemi ya Maadili mema kwa watoto. (Mapadre)

 

Sambamba na mada hizo zilizotolewa, kulikuwa na burudani mbalimbali kwa watoto kama vile ngoma, vichekesho, maigizo, muziki, ngonjela na nyimbo.

Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa waliofanya vizuri ili kuamsha ari ya kujiandaa vizuri wakati wa Kongamano.

 

Kwa upande wa Liturjia, watoto walihudumu vizuri na kwa zamu. Walishiriki vema katika Uimbaji wakati wa Misa, wengine walihudumu altareni na wengine walitumikia kwa nafasi mbalimbali wakati wa Misa. Siku ya kilele kulikuwa na maandamano yaliyoongozwa na Mhasham Askofu Msaidizi Godfrey Mwasekaga kuanzia Kanisa la kiaskofu Jimboni hadi Mwanjelwa. Tuliandamana vizuri bila kupata changamoto yeyote na kisha tukahitimisha kwa Misa Takatifu. Kwa ujumla vitu vyote vilifanyika vizuri bila kupata changamoto kubwa kwa watoto wetu.

Tunashukuru kwa miongozo mbali mbali tunayoipata kutoka Ofisi ya Taifa. Mungu awabariki.

 

 

Imeandaliwa na: Fr. Exavery Maingu Mafwimbo

Mkurugenzi PMS Jimbo Kuu la Mbeya