la Utoto Mtakatifu jimbo la Mbinga, lilifanyika toka tarehe 27-29/12/2024 Uaskofuni Mbinga. Jumla ya watoto 1267 na walezi 91 walishiriki kongamano hilo. Watoto na walezi wao waliripoti tarehe 27/12/2024, na tarehe 28/12/2024 siku ya Jumamosi mada nne zilitolewa.
Mada ya kwanza ilikuwa EKARISTI TAKATIFU, iliyotolewa na Padre Erasto Nyimbo ambaye ndiye Mkurugenzi wa PMS Jimbo la Mbinga.
Ikafuata MADA YA ULINZI WA MTOTO, iliyotolewa na Padre Joseph Ngahy mkurugenzi wa Miito Jimbo la Mbinga.
Mada ya tatu ilikuwa ni MAADILI, ilitolewa na Padre Leander Ndimbo mwalimu na mlezi wa Seminari ndogo Likonde jimbo la Mbinga.
Mwisho mada ya MIITO MITAKATIFU, ambayo ilitolewa na Sr. Filotea wa shirika la Masista wa Mtakatifu Vincent wa Paulo Mbinga na mkurugenzi wa miito wa Shirika hilo. Kila mada ilitolewa kwa muda wa saa moja.
Tarehe 29/12/2024 Kongamano lilifungwa likitanguliwa na maandamano toka kanisa la hija la Mtakatifu Alois Gonzaga Mbinga mjini kuelekea Kanisa kuu. Watoto walitembea umbali wa kilometa mbili na robo, na wakati wote wa maandamano watoto waliimba nyimbo mbalimbali. Baada ya maandamano, iliadhimishwa misa ya kufunga kongamano la Utoto Mtakatifu na kufungua Jubilei ya mwaka Mtakatifu, misa ambayo iliongozwa na Mhashamu John Chrisostom Ndimbo, Askofu wa jimbo Katoliki la Mbinga.
Imetayarishwa na: Pd. Erasto Nyimbo, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa (PMS)