Katika jimbo la Mpanda, kongamano lilianza tarehe 26 – 29 Desemba 2024. Tarehe 26 ilikuwa ni kwa ajili ya kuwasili. Tarehe 27 Des ilifanyika misa ya ufunguzi na bada ya hapo semina kwa watoto.

Watoto washiriki walikuwa 1,093, walezi 150, mapadre 12, masista 7 na Mha Baba Askofu na kufanyajumla kuu 1,263, ni sawa na ongezeko la asilimia 83 ya lengo kusudiwa.

Kwenye kongamano hilo, mada zilizotolewa ni mbili, ambazo ni;

  1. Unyanyasaji wa watoto – Pd Nicodemus Kyumana – Mkurugenzi wa PMS jimbo.
  2. Mazingira – Sr Mary Magdalene SND

 

Kilele cha kongamano kilikuwa tarehe 28 Desemba siku ya watoto mashahidi ambapo misa takatifu iliadhimishwa na Mha. Baba Askofu Eusebius Nzigilwa na kufuatiwa na chakuàla na burudani mbalimbali.

Tarehe 29 Desemba watoto walikuwa ni sehemu muhimu katika maadhimisho ya uzinduzi wa jubilei kuu kwa maandamano na misa takatifu iliyoadhimishwana Baba Askofu Eusebius Nzigilwa.

Baada ya Misa na chakula, na siku iliyofuata watoto walirudi maparokiani.

MAFANIKIO

  1. Ongezeko kubwa la ushiriki kwa watoto, walezi, mapadre na watawa.
  2. Ongezeko la ufahamu kwa watoto kutokana na mada wasilishwa.
  3. Ongezeko la hamasa la uundwaji wa kwaya za watoto.
  4. Ongezeko la ushiriki wa watoto wenye sare kwenye kongamano.

Tunamshukuru Mungu kwa ufanisi wa kongamano hili na tunatazamia maboresho na ufanisi mkubwa kwenye kongamano lijalo.

 

 

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Nicodemus Kyumana, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa- Jimbo