Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na baraka nyingi alizotujalia mwaka huu.Tunamshukuru pia kufanikisha uwepo wetu katika kongamano letu la Utoto Mtakatifu. Tunamshukuru mlezi wetu mkuu yaani Baba Askofu kwa kutupa nafasi ya kukua katika malezi kwani “mtoto ni malezi” Mwaka huu tulifanikiwa kuleta nyumbani wazo la Kongamano la tano la Ekarestia kitaifa kwa kuwakutanisha Watoto wapatao 933 na walezi 76 jumla 1009 kwenye viwanja vya uaskofuni kwa muda wa siku nne.
Aidha, mada zilizowasilishwa kwa watoto ni pamoja na: Undugu huponya ulimwengu (Na Mwl. Silvano), Imani Katoliki (Na Mwl. Festo Hiza), Mtoto Mmisionari na uwajibikaji – Elimu, Wajibu na matokeo yake (Na Mwl. Silvano)Namna ya kuishi maisha ya furaha ukiwa Mtoto (Na Mwl. Festo Hiza), Haki ya Mtoto mmisionari kwa Kanisa na Taifa (Na Mwl. Silvano) Maisha ya Mtoto mmisionari kwa Watoto wenzake (Na Mwl. Festo Hiza), Mashindano ya usomaji wa Biblia (Na Mwl. Silvano na Walezi Msista)
Walezi wa Utoto Mtakatifu walifundishwa ama kukumbushiwa juu ya Wajibu wa Mlezi katika Malezi (Na Mwl. Silvano)
MAFANIKIO
Watoto wamepata Malezi na mafundisho mblimbali kulingana na dhamira ya kongamano hususani Undugu unaoponya Ulimwengu na athari za kutokutambua haki za Mtoto. Walipata pia Sakramenti kama vile sakramenti ya Kitubio na Ekaresti Takatifu
MAPENDEKEZO YA WATOTO
- Watoto walipendekeza kuwa Walezi wawe na Kongamano lao wenyewe kutangulia kongamano la Watoto. Hii itawafanya kutoa malezi vizuri ikiwa wanajua wanachokifanya.
- Watoto walipendekeza kuwa Wazazi wasiwazuie Watoto wenzao kuja kongamano
- Watoto waliomba kuvumiliwa kwa usumbufu wao na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika malezi.
MWISHO
Siku ya kilele tulifanya Maandamano kabla ya adhimisho la Misa Takatifu ikiwa ni fursa kwa Watoto kuinjilisha kwa vitendo. Hakika tumeonja Uwepo wa Utukufu na Upendo wa Mungu kati ya Watoto na Walezi waliponywa na Yesu wa Ekaresti. Yote kwa Utukufu Wake.
Imeandaliwa na: Pd. Alphonce Ndaghine, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa – Jimbo