Watoto wa jimbo katoliki la Lindi wameweza kushiriki kongamano lao hapo Disemba  mwaka huu 2024, katika parokia ya Kilwa Masoko. Kongamano hili lilianza mnamo tarehe 26 – 28 Disemba (sikukuu ya watoto mashahidi). Washiriki watoto katika kongamano hili walikuwa jumla yao 410 kutoka katika kila parokia.

Katika kongamano hili watoto walifundishwa mada mbalimbali kama ifuatavyo: Jografia ya Biblia na Pd. Paul Chembe, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa Jimbo, Haki na wajibu wa mtoto na Pd. Fridolin Makwinya, Liturujia Ibada ya Misa Takatifu na Sr. Tereza Awino na mada juu ya Malezi ya Watoto iliwasilishwa na Mariam Mlacha.

Aidha katika kilele cha kongamano hilo, kulikuwa na maandamano ya watoto yaliyokuwa na lengo la kusambaza mbegu ya uinjilishaji, kwanza kwa watoto wengine ambao bado hawajamfahamu Mungu bado lakini pia kwa watu wote. Ni katika maamdamano haya, kwa bahati nzuri baba Askofu Wolfgang Pisa OFM Cap wa jimbo la Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, aliweza kufanya maandamano pamoja na watoto na kwa namna ya pekee kuongoza misa katika kilele cha kongamano hilo.  Hakika, katika kongamano hili ni dhahiri kabisa kuwa watoto walisia mbegu ya uinjilishaji, kwao binafsi na kwa wengine waliokuwa nje ya kundi hili.

 

 

 

Imeandaliwa na: Pd. Paul Chembe, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa-Jimbo